Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 05, 2024 Local time: 06:25

Mahathir ajiandaa kutekeleza mageuzi, kurejesha hadhi ya Malaysia


Malaysia Mahathir Mohamad
Malaysia Mahathir Mohamad

Waziri Mkuu wa Malaysia (92), Mahathir Mohamad, amedhamiria kurejesha hadhi ya nchi hiyo na urithi aliouacha, baada ya kuchukua tena madaraka kufuatia uchaguzi wa taifa uliofanyika mapema mwezi Mei.

Wakati wa utawala wake kwa kipindi cha miaka 22 miaka iliyopita, Mahathir alilijenga koloni dogo la zamani lililotawaliwa na Uingereza, kuwa moja ya nchi zilizokuwa na fahari ya uchumi wake katika bara la Asia.

Lakini baada ya kuondoka madarakani alishuhudia taifa hilo likiaibika na kugubikwa na kashfa za ufisadi ambazo zilikuwa zinafanana na maandishi ya mchezo wa filamu.

Katika mahojiano yake na VOA baada ya uchaguzi maridhawa uliopelekea kushindwa Waziri Mkuu Najib Razak, Mahathir alikuwa na msimamo thabiti katika kuleta mageuzi na kusema kuwa kipindi cha utawala wake uliopita kwa njia yoyote ile hakikuchangia kutokea utumiaji vibaya madaraka – kama vile shutuma zinazomkabili Najib.

“Hivyo basi, miaka 20 ya kwanza kama waziri mkuu ilikuwa kwa kiasi fulani ni mepesi. Nilirithi mfumo ambao tayari ulikuwepo. Yale ninayotakiwa kufanya ni kuanzisha mawazo mapya ili tuweze kuharakisha kukua kwa uchumi na maendeleo ya nchi ya Malaysia,” amesema juu ya kipindi hicho cha utawala wake ambacho kilimalizika 2003.

“Lakini hivi leo ninakabiliwa na nchi ambayo kwa kweli imeangamizwa,” ameongeza, akielezea kashfa za hivi karibuni.

Moja ya kashfa zinazovuma sana zinamhusisha Naji kwa upotevu wa mamilioni ya mamia ya dola kutoka katika mfuko wa serikali, unaojulikana kama 1 Malaysia Development Berhad, ambayo iliundwa mwaka 2009 kwa ajili ya miradi ya miundombinu na waziri mkuu aliyeshindwa katika uchaguzi.

Najib, ambaye amefikishwa mara kadhaa mbele ya Tume ya Kupambana na Rushwa ya Malaysia amekanusha kufanya kosa lolote.

XS
SM
MD
LG