Waziri Mkuu huyo wa zamani anayejulikana kwa utawala wake wa mabavu, na muungano wa vyama vya upinzani, Alliance of Hope, umekiondoa madarakani muungano wa chama cha Waziri Mkuu Najib Razak, Barisan National Coalition, kilichokuwa kimetawala Malaysia tangia nchi hiyo ipate uhuru mwaka 1957.
Kuchaguliwa kwake kunamfanya kuwa ni kiongozi mkongwe kuliko wote duniani.
Sherehe ya kuapishwa kwake imefanyika ikulu ya Kuala Lumpur na kumaliza uvumi uliokuwa unaenezwa kuwa chama cha Barisan National Coalition kingejaribu kunang'ania madarakani.
Mahathir, aliyekuwa amevalia vazi la utamaduni wa Malaysia na kofia ya Kiislam, aliapishwa na Mfalme Sultan Muhammad katika tafrija iliyofuata utamaduni wa nchi hiyo
Waziri Mkuu Najib Razak alikubali kushindwa Alhamisi, akisema yeye na wenzake katika chama "wamekubali uamuzi wa wananchi."