Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 17, 2024 Local time: 19:28

Mahakama yazima BBI Kenya


Nyuma: Jaji mkuu Martha Koome (katikati) akiwa na naibu wa jaji mkuu Philomena Mwilu, Jaji Smokin Wanjala Isaac Lenaola, Mohamed Ibrahim Njoki Ndungu na Jaji William Ouko wakati wa kikao cha maamuzi ya BBI katika mahakama kuu jiji Nairobi March 31, 2022. (Picha ya AFP)
Nyuma: Jaji mkuu Martha Koome (katikati) akiwa na naibu wa jaji mkuu Philomena Mwilu, Jaji Smokin Wanjala Isaac Lenaola, Mohamed Ibrahim Njoki Ndungu na Jaji William Ouko wakati wa kikao cha maamuzi ya BBI katika mahakama kuu jiji Nairobi March 31, 2022. (Picha ya AFP)

Mahakama ya juu nchini Kenya imetupilia mbali rufaa iliyokuwa imewasilishwa na serikali kuhusu marekebisho ya katiba maarufu kama BBI.

Jopo la majaji saba wakiongozwa na jaji mkuu Martha Koome, limetupilia mbali rufaa hiyo kwa msingi kwamba rais Uhuru Kenyatta, ambaye alianzisha mchakato wa BBI, hawezi kuanzisha machakato wa kurekebisha katiba kulinganana sheria za Kenya na hivyo mchakato mzima ulikiuka katiba ya nchi hiyo.

Mahakama imeamuru kuwa marekebisho ya katiba yanaweza tu kuanzishwa na bunge kupitia mchakato wa bunge kulingana na ibara ya 256 ya Katiba, au kupitia mchakato wa kura ya maamuzi kulingana na Ibara ya 257 ya katiba ya Kenya.

Jaji mkuu Martha Koome, jaji William Ouko, Isaac Lenaola, Philomena Mwilu, Mohammed Ibrahim, na jaji Smokin Wanjala, wamesisitiza kwamba ni lazima raia wa Kenya wahusishwe vikamilifu katika mchakato mzima wa kutaka kubadilisha katiba ya nchi hiyo.

Marekebisho ya katiba ya Kenya, BBI yalianzishwa na rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa chama cha Orange democratic movement ODM, Raila Odinga, kwa kile kilichotajwa kama hatua ya kuponya nchi hiyo kutokana na vidonda vya kisiasa vya mda mrefu ambapo mshindi katika uchaguzi mkuu anachukua madaraka na usimamizi wa ofisi zote za serikali.

Mabadiliko hayo vile vile yalikuwa na lengo la kuongeza ukubwa wa baraza la mawaziri, kuunda maeneo mengine 70 ya bunge, kuunda nafasi ya waziri mkuu ambaye angechaguliwa kutoka kwa wabunge, kuongeza kiasi cha pesa kwa serikali za kaunti, miongoni mwa mengine.

Imetayarishwa na Hubbah Abdi, VOA, Nairobi.

XS
SM
MD
LG