Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 30, 2025 Local time: 09:43

Mahakama yamwachilia waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan


Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Pakistan Shah-Mahmood Qureshi na waziri mkuu wa zamani Imran Khan
Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Pakistan Shah-Mahmood Qureshi na waziri mkuu wa zamani Imran Khan

Mahakama kuu ya Islamabad imebatilisha hukumu ya waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan na waziri wake wa mambo ya nje, Shah Mahmood Qureshi, katika kesi inayohusu kutolinda ipasavyo siri za serikali.

Katika taarifa fupi ya maelezo iliyoonwa na mwandishi wa VOA, majaji wawili wa Mahakama kuu walitangaza kuwaachilia huru Khan na Qureshi, huku ikikubali rufaa yao dhidi ya hukumu waliopewa.

Uamuzi huo unajiri baada ya mahakama ya chini kuwahukumu mwezi Januari Khan na Qureshi kifungo cha miaka 10 kila mmoja kwa kuweka hadharani maudhuwi ya waraka wa siri wa kidiplomasia uliotumwa na balozi wa Pakistan wa wakati huo kwenye Umoja wa mataifa.

Wawili hao walidai kuwa kesi hiyo ilichochewa kisiasa na kwamba kesi hiyo iliendeshwa kwa njia isio ya haki.

Licha ya uamuzi huo wa Mahakama kuu, Khan na Qureshi hawatarajiwi kuachiliwa huru. Khan ambaye anafungwa jela tangu mwezi Agosti mwaka jana, anatumikia kifungo cha hukumu ya kufunga ndoa isiyo halali.

Forum

XS
SM
MD
LG