Katika kesi hiyo baraza la mahakama limemkuta rais huyo na makosa ya udhalilishaji wa kijinsia, na kumkashifu mwandishi na kumtaka alipe fidia ya dola za kimarekani milioni 5.
Katika uamuzi wenye kurasa 59, jaji wa mahakama ya wilaya ya Marekani, Lewis Kaplan, mjini Manhattan, amesema baraza la mahakama halikufikia kutoa matokeo makali, na kwamba uamuzi wa Mei 9 haukuwa chini ya kiwango cha haki.
Carroll alimshutumu Trump, kuwa alimbaka katik chumba cha kubadilishia nguo katika duka moja la Manhattan katika miaka ya 1990, na baadaye kuzungumzia tukio hilo katika mtandao wa kijamii wa Trump, unoitwa Truth, kuwa ni uwongo wa kupandikiza hapo Oktoba 22.
Trump anadai kulipa fidia ya dola milioni 2 kwa udhalilishaji wa kijinsia ni fedha nyingi.
Forum