Baada ya miaka kadhaa ya ushawishi wa mataifa ya visiwa yaliyo hatarini kupotea kwa kuongezeka kwa kiwango cha bahari, baraza kuu la Umoja wa Mataifa liliiomba mahakama ya kimataifa mwaka jana kutoa maoni juu ya majukumu ya mataifa katika kuheshimu mabadiliko ya hali ya hewa.
Mwanasheria kiongozi wa taifa kisiwa cha Pasifiki Vanuatu, Margaretha Wewerinke-Sign, ameiambia The Associated Press kwamba wanataka mahakama hiyo kuthibitisha matendo yanayo haribu hali ya hewa kuwa ni kinyume cha sheria.
Tokea miongo kadhaa mpaka 2023, kiwango cha bahari duniani kimeongezeka kwa sentimita 4.3 baadhi ya sehemu za bahari ya Pacific ikiwa ni juu ya hapo.
Forum