Mahakama ya rufaa ya ufaransa imekataa ombi la Rwanda kumrudisha mjane wa hayati rais wa Rwanda Juvenal Habyarimana.
Waendesha mashitaka wa Rwanda wanasema mke huyo wa rais Agathe Habyarimana alihusika kwa kiasi kikubwa na mauaji ya halaiki ya 1994.
Maafisa wa Ufaransa walimkamata mwaka jana , baada ya Rwanda kutoa hati ya kumkamata wakimshitaki kwa mauaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya binadamu.
Waendesha mashitaka wa Ufaransa wamemshutumu mjane huyo kwa kushiriki mauaji baada ya mume wake kuuwawa wakati ndege yake ilipoangushwa karibu na mji mkuu wa Rwanda Aprili 6, 1994.