Mahakama ya rufaa kaskazini mwa Nigeria imefuta hukumu ya kifungo cha miaka 24 jela kwa mtu asiyeamini kuna Mungu kwa kosa la kukufuru na kupewa kifungo cha miaka mitano, mmoja wa mawakili wake aliliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumanne.
Kesi ya Mubarak Bala iliangazia suala lenye utata la kukufuru katika eneo linalokaliwa na Waislamu wengi kaskazini mwa Nigeria, ambako Sharia ya ki-islam inatumika sambamba na sheria za kawaida na ukosoaji kwa Uislamu ni nyeti sana.
Bala ambaye anaongoza taasisi inayoangazia masuala ya kibinadamu nchini Nigeria, alihukumiwa kifungo cha miaka 24 na mahakama kuu katika jimbo la Kano mwezi Aprili 2022 kwa ujumbe aliobandika kwenye mtandaoni kwa kipindi cha miezi kadhaa mwaka 2020 akiudhalilisha Uislamu, Mtume Muhammad na Mungu, kulingana na hati za mahakama ambazo shirika la habari la AFP imeziona.
Forum