Mahakama ya Moscow imemkamata mshukiwa mwingine kama mshirika katika shambulio lililofanywa na watu wenye silaha katika viunga vya Moscow kwenye tamasha moja ambalo liliuwa watu 144 mwezi Machi, kituo cha televisheni cha Moscow City Telegram kimesema Jumamosi.
Dzhumokhon Kurbonov, raia wa Tajikistan anatuhumiwa kwa kuwapatia washambuliaji njia za mawasiliano na ufadhili. Jaji katika Mahakama ya Wilaya ya Basmanny ya Moscow aliamua kwamba Kurbonov atazuiliwa kizuizini hadi Mei 22 akisubiri uchunguzi pamoja na kesi.
Shirika la habari la serikali ya Russia- RIA Novosti limesema Kurbonov alikamatwa Aprili 11 kwa siku 15 kwa mashtaka ya utawala wa ulanguzi wa magenge.
Shirika huru la habari la Russia, Mediazona limeeleza kuwa hii ni tabia ya kawaida inayotumiwa na vikosi vya usalama vya Russia kumshikilia mtu aliyeko kizuizini wakati kesi ya jinai ikiandaliwa dhidi yao.
Forum