Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 26, 2022 Local time: 15:03

Mahakama ya Mafisadi yawahukumu wawili kifungo cha maisha


Mahakama ya Mafisadi Tanzania yawahukumu Abdul Nsembo na mkewe Shamimu Mwasha kifungo cha maisha.Picha kwa Hisani ya Global Publishers TV, Tanzania.

Mahakama Kuu Kitengo cha Uhujumu Uchumi maarufu kama Mahakama ya Mafisadi, Dar es Salaam imewahukumu Jumatano kifungo cha maisha jela mfanyabiashara Abdul Nsembo (45) na mke wake Shamimu Mwasha (41) baada ya kukutwa na hatia ya makosa ya kujihusisha na dawa za kulevya aina ya Heroin.

Pia mahakama hiyo imetoa amri ya kutaifisha mali za watuhumiwa ikiwemo gari aina ya Discover 4 ili iwe mali ya Serikali, huku dawa hizo zikitakiwa kuteketezwa vimesema vyanzo vya habari nchini.

Hukumu ya kesi hiyo namba 4 ya mwaka 2020, imetolewa na Jaji Elinaza Luvanda baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili kati ya Jamhuri na Utetezi na kujiridhisha kwamba watuhumiwa wamekutwa na hatia katika makosa mawili ya usafirishaji dawa za kulevya.

Wawili hao walishtakiwa baada ya kudaiwa Mei Mosi, 2019 wakiwa eneo la Mbezi Beach, wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam kinyume na sheria ya uhujumu uchumi walikutwa na dawa hizo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG