Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 28, 2022 Local time: 00:54

Mahakama ya Kikatiba ya Angola yatupilia mbali rufaa ya upinzani


Kiongozi wa UNITA Adalberto Costa Junior.Angola, August 22, 2022. REUTERS/Siphiwe Sibeko. Reuters.

Mahakama ya Kikatiba ya Angola ilifanya uamuzi wa mwisho siku ya Alhamisi kutupilia mbali malalamiko yaliyowasilishwa na mgombea urais aliyeshika nafasi  pili katika uchaguzi wa Agosti 24 akitaka kubatilishwa kwa matokeo yaliyokipa ushindi chama tawala cha MPLA.

Baada ya uchaguzi wa nchi hiyo uliokuwa na ushindani mkali tume ya uchaguzi ilitangaza wiki iliyopita Chama cha People's Movement for the Liberation of Angola (MPLA) kuwa mshindi, na kuongeza muda wa takriban miongo mitano ya utawala wake usioingiliwa na kumpa Rais Joao Lourenco muhula wa pili.

Zaidi kidogo ya asilimia 51 ya wapiga kura walikiunga mkono chama cha MPLA. Chama cha Total Independence of Angola (UNITA), wapinzani wa muda mrefu na adui wa zamani wa vita vya wenyewe kwa wenyewe, kilichukua takriban asilimia 44 ikiwa ni matokeo yake bora zaidi kwenye rekodi yao kulingana na tume hiyo.

Kiongozi wa UNITA Adalberto Costa Junior aliyapinga matokeo hayo, akitaja hitilafu kati ya hesabu za tume na hesabu za chama chenyewe. Aliishutumu tume ya uchaguzi, ambayo inadhibitiwa zaidi na MPLA, kwa udanganyifu.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG