Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 04:21

Mahakama ya Juu ya Thailand imemuachia huru Yingluck Shinawatra


Waziri Mkuu wa zamani wa Thailand, Yingluck Shinawatra akiwasalimia wafuasi wake katika mahakama mjini Bangkok, Thailand. August 1, 2017. REUTERS/Athit Perawongmetha
Waziri Mkuu wa zamani wa Thailand, Yingluck Shinawatra akiwasalimia wafuasi wake katika mahakama mjini Bangkok, Thailand. August 1, 2017. REUTERS/Athit Perawongmetha

Yingluck alishutumiwa kwa kutoendesha mchakato sahihi wa zabuni katika Roadshow to Build the Future of Thailand

Mahakama ya Juu ya Thailand leo Jumatatu imemuachia huru Waziri Mkuu wa zamani Yingluck Shinawatra kwa shutuma za ufisadi kwa kutoa kandarasi ya serikali wakati akiwa madarakani. Yingluck ambaye alitawala kuanzia mwaka 2011 hadi alipoondolewa madarakani katika mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2014 alishtakiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi katika mradi wa mwaka 2013 wenye thamani ya zaidi ya dola milioni 6.7.

Uamuzi huo ni mafanikio ya hivi karibuni ya kisheria kwa familia yenye nguvu ya Shinawatra baada ya kaka yake Yingluck Thaksin, Waziri Mkuu wa mara mbili ambaye pia aliondolewa madarakani kwa njia ya mapinduzi, aliachiliwa huru kwa msamaha mwezi Februari, miezi sita katika kile ambacho awali kilikuwa kifungo cha miaka minane jela.

Yingluck na watu wengine watano walishutumiwa kwa kutoendesha mchakato sahihi wa zabuni katika “Roadshow to Build the Future of Thailand” kampeni ya kukuza miradi ya miundombinu ya serikali yake.

Majaji tisa walioketi katika mahakama ya juu ya ufalme huo waliamua kwa kauli moja kumpendelea Waziri Mkuu huyo wa zamani, wakisema hawana nia yoyote ya kuvinufaisha vyombo viwili vikuu vya habari ambavyo vilishinda mkataba huo, kulingana na taarifa.

Forum

XS
SM
MD
LG