Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 19, 2024 Local time: 16:32

Mahakama ya juu ya Kenya yahalalisha ushindi wa Ruto


William Ruto baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa Agosti 9 na IEBC
William Ruto baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa Agosti 9 na IEBC

Mahakama ya juu nchini Kenya leo imekubaliana na maamuzi ya tume ya uchaguzi na mipaka IEBC kuwa ushindi wa William Ruto katika uchaguzi wa rais hapo Agosti 9 ulikuwa halali, na kumaliza wiki kadhaa za hali kutokuwa na uhakika wa kisiasa.

Imekuwa ni pigo kubwa kwa raila Odinga ambaye aliwasilisha changamoto mahakamani akidai kulikuwa na ubadhirifu katika upigaji kura. Huu ni uamuzi wa pamoja, kesi zilizowasilishwa zimefutwa, kama ilivyotangazwa mara ya kwanza kuwa Ruto ni rais mteule, amesema jaji mkuu Martha Koome.

Odinga aliwasilisha changamoto mahakama ya juu mwezi uliopita, akidai alikuwa na ushahidi wa kutosha kuonyesha kuwa kwa hakika alishinda uchaguzi.

Wote Ruto na Odinga waliahidi kuwa wataheshimu uamuzi wa mahakama.

XS
SM
MD
LG