Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 21, 2025 Local time: 17:13

Mahakama ya juu Marekani imetoa njia ya utoaji mimba wa dharura kwa Idaho


Jengo la Mahakama ya Juu Marekani
Jengo la Mahakama ya Juu Marekani

Uamuzi huo umekuja baada ya siku moja kufuatia maoni yaliyochapishwa kwa muda mfupi kwenye tovuti ya mahakama hiyo.

Mahakama ya Juu Marekani ilitoa njia leo Alhamisi kwa hospitali za Idaho kutoa huduma za dharura za utoaji mimba kwa wakati huu, katika uamuzi wa kiutaratibu ambao uliacha maswali muhimu bila majibu na inaweza kumaanisha kwamba suala hilo linaishia hapo kabla ya mahakama iliyojaa wa-Conservative kukutana hivi karibuni.

Uamuzi huo umekuja baada ya siku moja kufuatia maoni yaliyochapishwa kwa muda mfupi kwenye tovuti ya mahakama hiyo kwa bahati mbaya, na kuondolewa haraka, lakini sio kabla ya kuonekana kwenye Bloomberg News.

Maoni ya mwisho yanaonekana kwa kiasi kikubwa sawa na rasimu iliyotolewa mapema. Inabadilisha amri ya awali ya mahakama ambayo ilikuwa imeruhusu marufuku ya utoaji mimba kwa Idaho kuanza kutumika, hata katika dharura za matibabu.

Forum

XS
SM
MD
LG