Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 07:42

Walioua waislamu India wahukumiwa


Mahakama ya India leo imehukumu watu 26 kutokana na kuuwawa kwa waislamu 69 na kundi la kihindi kwenye jimbo la Gujarat nchini India mwaka wa 2002.

Kumi na moja kati yao wameshitakiwa na mauwaji yalioshuhudiwa kwenye ghasia za miezi mitatu na ambazo ziliacha zaidi ya watu 1,000 wakiwa wamekufa miaka 14 iliopita.

Miongoni mwa watu 69 waliokatakatwa hadi kufa wakati wakichukua hifadhi kwenye nyumba ya makazi mjini Ahmedabad, ni aliekuwa mjumbe wa baraza la congress Ehsan Jafri.

Mke wa Jafri amefurahishwa na uamuzi wa mahakama lakini hakufurahia kuachiliwa kwa washukiwa 36 miongoni mwa walioshitakiwa.

Tangu 2002, zaidi ya watu 100 wamehukumiwa kutokana na ghasia hizo lakini bado kuna kesi nyingi ambazo hazijasikilizwa. Hukumu ya washukiwa 24 itatolewa jumatatu na wale 11 walioshitakiwa kwa mauwaji huenda wakahukumiwa kifo iwapo watapatikana na hatia.

XS
SM
MD
LG