Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 04, 2024 Local time: 00:15

Mahakama yamhukumu Mladic kifungo cha maisha


Ediba Salihovic, kulia, anyoosha mikono kuonyesha faraja baada ya mahakama kutoa hukumu dhidi Ratko Mladic karibu na mji wa Srebrenica, Bosnia.
Ediba Salihovic, kulia, anyoosha mikono kuonyesha faraja baada ya mahakama kutoa hukumu dhidi Ratko Mladic karibu na mji wa Srebrenica, Bosnia.

Majaji wa jopo la uhalifu wamemhukumu kiongozi wa zamani wa jeshi la Bosnia, Ratko Mladic, kutumikia kifungo cha maisha.

Mladic amepatikana na hatia ya mauaji ya halaiki, uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.

Mauaji haya yalitokana na vita vya miaka ya 90 katika nchi iliyojulikana kama Yugoslavia. Mahakama hiyo imemkuta na hatia kwa makosa 10.

Mladic, anayejulikana kama “Chinjachinga wa Bosnia,” ni kiongozi wa mwisho wa kijeshi kukabiliwa na tuhuma za jinai katika mahakama hiyo maalum, iliyowekwa kushughulikia na mauji ya vita vya Bosnia vilivyoshamiri kutoka mwaka 1992 hadi 1995.

Mladic, ambaye amekuwa akikabiliwa na mashtaka hayo tangu 2012, ametuhumiwa na makosa ya mauaji ya halaiki 11, jinai za kivita dhidi ya ubindamu kwa madai ya kuhusika kwake kuongoza kampeni ya kuwaua kwa kuvizia kwa risasi watu huko Sarajevo.

Mauaji ya 1995 ya zaidi ya Waislam wanaume na wavulana 8,000 huko Srebrenica – mauaji mabaya kuliko yote yaliyowahi kutokea Ulaya tangu Vita vya Dunia II.

Waendesha mashtaka katika kesi wameitaka Mahakama ya Kimataifa The Hague (ICT) kumpa adhabu ya kifungo cha maisha Mladic.

XS
SM
MD
LG