Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 14:35

Mahakama Kenya yasitisha vipengele vya sheria ya usalama


Mswaada wa sheria mpya ya usalama ulipitishwa na bunge hivi karibuni mjini Nairobi
Mswaada wa sheria mpya ya usalama ulipitishwa na bunge hivi karibuni mjini Nairobi

Mahakama Kuu nchini Kenya imesitisha kwa muda vipengele muhimu vyenye utata kwenye sheria mpya ya usalama wa taifa na mpaka uchunguzi kamili ufanyike kuhusu sheria hizo.

Jaji wa mahakama ya kuu, George Odunga alisema Ijumaa kwamba sheria hiyo mpya inayopinga ugaidi ilizusha wasi wasi kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu.

Hatua hiyo inafuatia changamoto za kisheria zilizotolewa na upinzani nchini Kenya.

Baada ya kutia saini mswaada wenye utata uliopitishwa na bunge mwishoni mwa mwaka jana, Rais Uhuru Kenyatta alisema mwezi uliopita kwamba sheria hiyo inaipa nchi baadhi ya mbinu zinazohitajika ili kupambana na kitisho cha ugaidi.

Vipengele vya sheria ya usalama nchini Kenya viliongeza muda wa kushikiliwa kwa washukiwa bila kufunguliwa mashtaka kwa siku 360 kutoka siku 90 zinazotekelezwa hivi sasa na kuweka sheria kali juu ya namna vyombo vya habari vinavyoweza kuripoti taarifa za usalama.

Wabunge wanaokosoa sheria hii Gladys Wanga(L) na Christine Mbaya Dec. 18, 2014.
Wabunge wanaokosoa sheria hii Gladys Wanga(L) na Christine Mbaya Dec. 18, 2014.

Wakosoaji wanasema hatua hizo zinatishia uhuru wa raia na uhuru wa kujieleza.

Rais wa Kenya alisema watu waliohusika na harakati za uhalifu ndio pekee wanatakiwa kuwa na khofu na sheria hii.

Ushirika wa muungano wa Jubilee ambao ndio unaongoza serikali ya Kenya ulishinikiza mswaaada huu kama njia bora ya kuiwezesha nchi kupambana na ugaidi ambao unahusisha zaii wanamgambo wa kundi la al-Shabaab wenye makao makuu yake nchini Somalia.

Nchi tisa za magharibi ikiwemo Marekani walielezea wasi wasi wao kuhusu mswaada huo katika taarifa ya mwezi uliopita wakisema wanaunga mkono mipango ya kuimarisha usalama lakini sio katika kuhatarisha muingiliano wa haki za binadamu.

XS
SM
MD
LG