Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 22:40

Mahakama Kenya yamkuta na hatia  mwanadiplomasia wa Venezuela


Jengo la mahakama mjini Nairobi, Kenya.
Jengo la mahakama mjini Nairobi, Kenya.

Mahakama moja ya Kenya siku ya Jumatano ilimkuta na hatia  mwanadiplomasia wa Venezuela kwa  kumuua kaimu balozi wa taifa hilo la Amerika Kusini muongo mmoja uliopita nyumbani kwake katika ujirani karibu na mjini  Nairobi.

Dwight Sagaray, ambaye alikuwa katibu kiongozi katika ubalozi huo, alikutwa na hatia ya mauaji ya Olga Fonseca Julai 2012, Jaji Roselyn Korir alisema katika uamuzi wake.

Mahakama pia iliwatia hatiani raia watatu wa Kenya waliokuwa wameshtakiwa pamoja na Sagaray, ikisema walihusika katika mpango wa pamoja wa kutekeleza mauaji hayo.

Mshukiwa mwingine aliyekimbia baada ya mauaji hayo bado yuko huru na mahakama ilisema hati yake ya kukamatwa iendelee kutumika.

Sagaray, ambaye alivalia suti na tai kizimbani, alifunika uso wake wakati hukumu hiyo iliposomwa.

XS
SM
MD
LG