Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 10, 2024 Local time: 19:29

Mahakama Japan yasema kutoruhusu ndoa za jinsia moja ni kinyume cha katiba


Watu wakiwa na mawakili wao wakibeba mabango na bendera kuunga mkono maamuzi ya mahakama ya chini kwamba kutoruhusu ndoa za jinsia moja ni kinyume cha katiba.
Watu wakiwa na mawakili wao wakibeba mabango na bendera kuunga mkono maamuzi ya mahakama ya chini kwamba kutoruhusu ndoa za jinsia moja ni kinyume cha katiba.

Mahakama moja nchini Japan imetoa maamuzi Jumanne kuwa kutoruhusu ndoa za jinsia moja ni kinyume cha katiba.

Uamuzi huo umepokelewa kwa shangwe na wanaharakati ikiwa ni hatua kuelekea haki sawa katika ndoa katika Kundi la Group of Seven pekee ambalo halina haki ya kisheria kuwalinda wanaokuwa katika uhusiano wa jinsia moja.

Uamuzi wa Mahakama ya Wilaya ya Nagoya ulikuwa wa pili kuona marufuku ya ndoa ya jinsia moja ni kinyume cha katiba, kati ya kesi nne zilizosikilizwa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, kuna uwezekano ikaongeza shinikizo kubadilisha sheria katika nchi ambayo katiba inasema ndoa ni kati ya mwanaume na mwanamke.

“Uamuzi huu umetuokoa kutoka maumivu tuliyopata katika uamuzi wa mwaka jana uliosema kuwa hapajakuwa na kosa lolote na upigaji marufuku wa hilo, na maumivu ya yale serikali inaendelea kuyasema,” wakili Yoko Mizutani aliwaambia waandishi wa habari na wanaounga mkono ndoa ya jinsia moja nje ya mahakama.

Wakili huyo alikuwa anazungumzia uamuzi uliotolewa huko Osaka mwaka 2022 kuwa marufuku hiyo ya ndoa ya jinsia moja ilikuwa haiko nje ya katiba.

Baadaye mahakama moja mjini Tokyo iliendeleza marufuku ya ndoa ya jinsia moja lakini ikasema kukosekana sheria ya kuzilinda familia za jinsia moja kunakiuka haki zao za binadamu.

Uamuzi wa Jumanne ulipokelewa kwa furaha kutoka kwa wanaharakati na wanaounga mkono ndoa hizo wakipeperusha bendera za upinde wa mvua nje ya mahakama hiyo.

Japokuwa maoni yanaonyesha asilimia 70 ya umma unaunga mkono ndoa za jinsia moja, chama tawala cha waconservative cha Liberal Democratic cha Waziri Mkuu Fumio Kishida kinapinga hilo.

Kishida mwezi Februari alimfukuza kazi msaidizi wake aliyesababisha hasira kwa kusema kuwa watu wataikimbia Japan iwapo ndoa ya jinsia moja itaruhusiwa, lakini Waziri Mkuu aliendelea kuchukua msimamo wa kutoiunga mkono ndoa hiyo na amesema mjadala lazima uendelee “kwa tahadhari.”

Hata hivyo, zaidi ya manispaa 300 ambazo asilimia 65 ya watu wanaishi humo zinaruhusu mahusiano ya jinsia moja ili kuingia katika mikataba,

Forum

XS
SM
MD
LG