Hati ya mashitaka imeonyesha kuwa Khama alishtakiwa pamoja na watu wengine watatu, tovuti binafsi ya Mmegi imeripoti.
Yeye na mkuu wa upelelezi wa zamani Isaac Kgosi , kamishna wa polisi wa zamani Keabetswe Makgophe na makamu katibu mkuu mstaafu Bruno Pledi wanakabiliwa na jumla ya mashitaka 38 yakiwemo kupatikana na silaha kinyume cha sheria, kumiliki silaha kinyume cha sheria na wizi wa bunduki.
Nchini Botswana kumiliki silaha kinyume cha sheria kunaweza kusababisha kifungo cha hadi miaka 10 jela.
Khama hapo awali aliliambia gazeti la Afrika Kusini la Daily Maverick kwamba anahifadhi bunduki zake za kuwindia, na aina nyingine zilizoko nyumbani kwake kwa zaidi ya miongo mitatu.
Baadhi ya haya yalikuwa maelezo yake rasmi na binafsi ya usalama , alinukuliwa akisema.