Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 15:26

Rais Magufuli akutana na Maalim Seif


Rais Magufuli akutana na Maalim Saif
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:16 0:00

Rais Magufuli akutana na Maalim Saif

Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli amekutana na kiongozi wa upinzani na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maalim Seif Sharrif Hamad, Jumatatu Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Maafisa wa ikulu wanaeleza kwamba viongozi hawa wamejadili hali ya kisiasa Zanzibar na wamefurahishwa na hali ya usalama na utulivu inayoendelea. Baada ya mazungumzo yao ya faragha walizungumza na waandishi wa habari ambapo Rais Magufuli amewapongeza rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein, Makamu wake Maalim Seif Sharif Hamad, na viongozi wote wanaoshiriki katika mazungumzo ya kuleta hali ya uelewano Zanzibar.

Rais Magufuli pia amewapongeza na kuwashukuru wananchi wa Zanzibar kwa kudumisha amani na utulivu wakati wa mazungumzo baina ya viongozi wa CUF na CCM yakiendelea huko Zanzibar.

Katika Mazungumzo hayo Rais Magufuli amemshukuru Makamu huyo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kwa taarifa yake huku akimsihi waendelee na mazungumzo hadi suluhisho muafaka lipatikane.

Majadiliano yanayoendelea yanatoa fursa ya kudumishwa kwa utulivu na sifa njema ya nchi yetu. Wote kwa pamoja wamewaomba wananchi waendelee kuwa watulivu ili kutoa nafasi ya majadiliano yanayoendelea kufikia hatma njema. Wameelezea matumaini yao kuwa vyama vya CCM na CUF haviwezi kushindwa kupata suluhu ya mgogoro huo.

Rais Magufuli amemuhakikishia kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano itahakikisha kuwa amani na utulivu unaendelea kudumishwa Zanzibar.

XS
SM
MD
LG