Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 03, 2022 Local time: 07:59

Nchi inatakiwa kuwa na uchumi wa viwanda - Magufuli


Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli akisisitiza kupambana na rushwa na kupunguza matumizi yasiyo ya lazima katika serikali.

Katika kuadhimisha mwaka mmoja wa uongozi wake wa awamu ya tano rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amesema ataendelea kuhakikisha nchi hiyo inakwenda kwa kupambana na wala rushwa na watendaji wabomu ili nchi ifikie uchumi wa viwanda kama alivyoahidi.

Rais Magufuli, Ijumaa amefanya mkutano na wahariri na waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali vya habari nchini Tanzania kuzungumzia tathmini ya mwaka wake mmoja madarakani huku akipuuza madai kwamba anaendesha nchi kibabe kwa kuminya demokrasia na kwamba anachokifanya ni kupambana na mfumo mbovu ulioyumbisha maendeleo ya nchi.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:22 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Akizungumza kuhusiana na mchakato wa katiba mpya Rais Magufuli amesema kwa wakati huu anapigana kuona nchi inakwenda kwenye maendeleo huku akisistiza kwamba suala la katiba litakuja baadaye.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG