Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 05, 2023 Local time: 23:06

Magufuli awasamehe wafungwa 61 waliohukumiwa kifo


Rais John Magufuli

Rais wa Tanzania John Magufuli ametoa msamaha kwa wafungwa 61 waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari nchini Tanzania idadi ya walioachiwa huru wakiwemo wenye kutumikia vifungo ni 1,821 ambao amri hiyo ya rais inataka waachiliwe huru mara moja.

Kadhalika wafungwa 8157 wamepunguziwa adhabu zao. Idadi hiyo ya msamaha kwa wafungwa inatajwa kuwa ni kubwa kuliko katika awamu zilizopita na hasa zinazo wahusisha wafungwa wa kunyongwa na vifungo vya maisha.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Parole, Augustine Mrema amepongeza uamuzi wa Rais John Magufuli wa kutoa msamaha kwa wafungwa na kumuelezea kama Rais mwenye upendo wa aina yake.

Akizungumza na gazeti la Mwananchi Jumamosi, Mrema amesema ni wazi kuwa Rais amesikia kilio cha watu na kuamua kufanya ubinadamu ili kupunguza msongamano wa wafungwa magerezani.

“Magerezani kuna uozo, wapo watu wengine wanajaa kule kwa makosa ambayo wanaweza kulipa faini tu wakatoka, nilianzisha kampeni ya kuwalipia faini wafungwa ambao walishindwa kujilipia lakini kutokana na maslahi ya baadhi ya watu nikaambiwa nisitishe kwa madai kuwa wafungwa hao hawajajutia makosa," amesema Mrema.

Ameongeza kuwa: "Naomba watu wa magereza wabadilike hakuna sababu ya kuwajaza wafungwa ambao wanatakiwa kutoka..."

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG