Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 06:43

Magufuli afanya mabadiliko baraza la mawaziri


Waziri wa Mambo ya Ndani wa zamani Mwigulu Nchemba
Waziri wa Mambo ya Ndani wa zamani Mwigulu Nchemba

Rais John Magufuli wa Tanzania amefanya mabadiliko madogo katika baraza lake la mawaziri ambapo amemteua aliyekuwa naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Kangi Alphaxard Lugola kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, kuchukua nafasi ya Mwigulu Nchemba.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi nafasi ya naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais inachukuliwa na Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini, Musa Ramadhani Sima.

Pia Rais ameongeza nafasi ya uteuzi wa Naibu Waziri katika Wizara ya Kilimo kutokana na umuhimu wa Wizara hiyo ambapo, Mbunge wa Morogoro Kusini, Omary Mgumba ameteuliwa kushika nafasi hiyo.

Katika mabadiliko hayo madogo, Rais Magufuli amefanya uhamisho wa Waziri Makame Mbarawa kutokea Wizara ya Ujezni na Uchukuzi na sasa anakuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji, huku aliyekuwa katika wizara hiyo, Mhandisi Isack Kamwelwe anakuwa Waziri wa Uchukuzi.

XS
SM
MD
LG