Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 07, 2023 Local time: 14:35

Magaidi 11 wauwawa Pakistan


Pakistan, Alhamisi imesema shambulio la kijeshi dhidi ya ugaidi katika eneo la mbali karibu na mpaka wa Afghanistan limewaua wanamgambo 11.

Wanamgambo hao wanaohusishwa na kundi lililopigwa marufuku la msimamo mkali.

Operesheni yenye msingi wa kijasusi katika wilaya ya Waziristan Kusini ilifanikiwa kuzuia ugaidi wa hali ya juu, taarifa ya kijeshi ilisema.

Duru za usalama zilisema watu waliouawa, wakiwemo washambuliaji wa kujitoa mhanga na kamanda mkuu, walikuwa wanachama wa Tehrik-i-Taliban Pakistan (TTP), au Taliban ya Pakistani.

Kundi hilo linaendesha shughuli za ugaidi nchini Pakistani, ikilenga zaidi vikosi vya usalama na raia.

TTP imeua mamia ya watu, vikiwemo vikosi vya usalama, katika mwaka uliopita.

Zaidi ya vikosi 40 vya usalama vya Pakistan viliuawa mwezi Disemba pekee, ambao uligeuka kuwa mwezi mbaya zaidi katika muongo mmoja wa ghasia za kigaidi nchini humo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG