Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 11:22

Mafuvu 17 ya watu yagundulika katika nyumba inayoshukiwa ya ibada Uganda


Kijiji cha Kabanga kiko jirani na mji wa Mpigi, takribani kilometa 40 Magharibi mwa Kampala
Kijiji cha Kabanga kiko jirani na mji wa Mpigi, takribani kilometa 40 Magharibi mwa Kampala

Mafuvu ya watu kumi na saba yaliyokuwa yamezikwa ndani ya makasha ya chuma yamefukuliwa katika jengo linaloshukiwa kuwa la Ibada katikati mwa Uganda, polisi wameliambia shirika la habari la AFP.

Watoto waliokuwa wakitafuta kuni nje ya kijiji cha Kabanga jirani na mji wa Mpigi, takribani kilometa 40 magharibi mwa mji mkuu Kampala, walifanya ugunduzi huo wa kutisha siku ya Jumatatu, kulingana na vyombo vya habari vya ndani.

Polisi wamesema wakazi waliwaambia maafisa kuwa kulikuwa na maboksi yaliyokuwa na vitu vinavyoonekana kuwa mafuvu yaliyozikwa ndani ya jengo la ibada.

“Haraka tuliingia na kuchimba eneo hilo, na mpaka sasa tumepata mafuvu ya binadamu 17” msemaji wa polisi wa eneo hilo Majid Karim alisema.

“Tunafanya uchimbaji zaidi kuhakikisha hakuna mafuvu zaidi kuliko haya tuliyoyagundua” alisema.

Aliongeza kuwa mabaki hayo yanafanyiwa uchunguzi kujua umri wao na jinsia, pamoja na kujua lini yalifukiwa.

Amewasihi watu kuwa watulivu, akisema baadhi ya wakazi wameondoka kwa woga.

Forum

XS
SM
MD
LG