Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 12, 2024 Local time: 03:16

Mafuriko yaua watu 54 nchini Chad


Ramani ya Chad
Ramani ya Chad

Mafuriko katika jimbo la kaskazini mashariki mwa Chad la Tibesti yaliua watu 54, maafisa walisema.

Mafuriko hayo yaliyosababishwa na mvua ilionyesha kuanzia Ijumaa hadi Jumatano yalisomba pia maelfu ya maduka na magari, alisema Jumatano Mahamat Tochi Chidi, gavana wa jimbo la Tibesti.

Mvua inayoendelea kunyesha ni tukio la hali ya hewa ambalo huikumba kanda hiyo kila baada ya miaka mitano hadi 10, alisema Idriss Abdallah Hassan, mkuu wa idara ya taifa ya hali ya hewa.

Wengi miongoni mwa waliofariki na kutoweka wanadhaniwa kuwa ni wachimba dhahabu wa kigeni wanaofanya kazi katika jimbo hilo kwa njia isio halali, alisema Brahim Edji Mahamat, mkuu wa shirika la kiraia katika eneo hilo.

Borkou-Ennedi-Tibesti, eneo linalozunguka majimbo matatu ya kaskazini mwa Chad na kufika hadi kwenye mpaka na Libya, ni eneo kubwa la jangwa la milima.

Forum

XS
SM
MD
LG