Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 23:03

Mafuriko Uganda yawakosesha makazi watu 7,000


Magari yakijaribu kupita katika barabara iliyofurika maji mjini Jinja, Uganda
Magari yakijaribu kupita katika barabara iliyofurika maji mjini Jinja, Uganda
Mvua kubwa inaonyesha katika maeneo ya kusini- magharibi mwa Uganda inasababisha mafuriko makubwa kwenye maeneo ya mlima Ruwenzori na kusababisha kufurika kwa mto Nyamwamba na kupelekea miji na vijiji ya wilaya ya Kasese kuzama kwa maji.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:00 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Akizungumza na Sauti ya Amerika, Waziri wa masuala ya majanga nchini Uganda, Musa Echweru alisema kuwa kiasi cha watu 7,000 wamekoseshwa makazi kufuatia mafuriko hayo na pia kuna idadi ya vifo vya watu sita wakiwemo watoto.

Waziri Echweru aliyetembelea maeneo ya mafuriko amesema serikali ya Uganda imetoa vifaa vya dharura na chakula kwa watu walioathirika na mafuriko hayo. Pia alisema wanajaribu kufanya kazi na jeshi la taifa, UPDF ili kupata njia ya kuweka uzio kwenye ukingo wa mto Nyamwamba na kulazimisha maji kurudi kufuata mkondo wake.

Wakati huo huo Waziri Echweru anaonya uwezekano wa kutokea mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu katika wilaya hiyo. Serikali ya Kampala inatarajiwa kukutana kwa kikao cha dharura kujadili tatizo la watu walokoisoshwa makazi huko Kasese.
XS
SM
MD
LG