Afisa wa polisi wa ngazi ya juu pamoja na mwenzake wameuawa kwa kuchomwa visu Jumatatu usiku.
Mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 3 aliokolewa na polisi, na mshambuliaji kwa jina Larossi Abballa ameuwawa na polisi.
Watu wawili wanaohusishwa na wamekamatwa wakati uchunguzi ukiendelea kutokana na vifo hivyo.
Rais wa Ufaransa, Francois Hollande, amesema mauwaji hayo ni ya kigaidi na yametokea wakati nchi yake ikiwa imeimarisha usalama ikiwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Euro 2016.
Abballa alikuwa amehukumiwa kifungo cha miaka 3 jela mwaka wa 2013 kwa kutoa mafunzo kwa wapiganaji wa jihad nchini Pakistan. Chombo cha habari cha Islamic State cha Amaq kimedai kuhusika kwenye shambulizi hilo ingawa halijadhibitisha rasmi iwapo lina uhusiano na mshambuliaji.