Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 15:21

Mtuhumiwa wa usafirishaji wa binadamu atetewa na familia


Marafiki pamoja na jamii ya Meritrea aliyezuiliwa Italy kwa madai ya kusafirisha wahamiaji haramu wanasema kuwa polisi wanamzuilia kimakosa kwa kuwa si yeye.

Polisi wa Italy wamesema Jumatano kuwa Medhanie Yehdego Mered amezuiliwa nchini humo baada ya kusafirishwa kutoka Sudan. Hata hivyo vyanzo vinasema kuwa mtu alieshikiliwa ni Meritrea mwingine kwa jina Medhanie Tesfamariam Berhe.

Amanuel Zaid aliefanya kwenye kituo kimoja cha televisheni cha Eritrea na anayeishi katika jimbo la Virginia hapa Marekani ameambia VOA kuwa ametumia muda wa siku nne akipiga simu Sudan kutafuta rafiki yake wa siku nyingi na jirani mjini Asmara.

Berhe anasemekana kuwa mwenye umri wa miaka 22 huku Mered anaeaminika kufanya biashara hiyo haramu ya kusafirisha wahamiaji akiaminika kuwa mwenye umri wa miaka 35.

XS
SM
MD
LG