Mazishi ya Jumamosi yalifanyika huku idadi ya vifo kutokana na ajali hiyo ya boti ya wahamiaji ikiongezeka na kufikia 89 na kuifanya kuwa mbaya zaidi kufikia sasa huku idadi kubwa ya watu wakikimbia Lebanon inayokumbwa na mzozo wa kiuchumi.
Jeshi la Lebanon lilitangaza kuwa wanajeshi wamemkamata mtu mmoja anayedaiwa kuandaa safari hiyo iliyouwa watu. Mzozo wa kiuchumi wa miaka mitatu wa Lebanon unachukuliwa kuwa mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa duniani tangu miaka ya 1850 na kusababisha robo tatu ya nchi hiyo kuwa maskini.