Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 18, 2024 Local time: 07:07

Maelfu ya walowezi wa Israel wavamia eneo la kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi


Kiongozi wa chama cha Likud na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akiwasalimia wafuasi wake katika makao makuu ya chama chake wakati wa uchaguzi mkuu wa Israel mjini Jerusalem, Novemba 2, 2022.
Kiongozi wa chama cha Likud na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akiwasalimia wafuasi wake katika makao makuu ya chama chake wakati wa uchaguzi mkuu wa Israel mjini Jerusalem, Novemba 2, 2022.

Maelfu ya walowezi wa Israel wamevamia eneo la kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi Jumapili jioni na kuchoma moto magari na nyumba baada ya walowezi wawili kuuawa na mshambuliaji wa Kipalestina.

Maafisa wa Palestina wanasema mtu mmoja ameuawa na wengine wanne kujeruhiwa vibaya. Mauaji hayo ya risasi, yalifuatiwa na shambulio la usiku wa manane, yanaibua maswali kuhusu tamko la Jordan kwamba ilipokea uhakikisho kutoka kwa waisrael na Wapalestina kutuliza wimbi la ghasia lililodumu kwa mwaka mzima.

Vurugu hizo zilitokea muda mfupi baada ya serikali ya Jordan, ambayo ilikuwa mwenyeji wa mazungumzo ya Jumapili kwenye eneo la mapumziko la Bahari ya Sham la Aqaba, kusema pande zote zimekubaliana kuchukua hatua za kupunguza mivutano na zitakutana tena mwezi ujao kabla ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa waislamu.

XS
SM
MD
LG