Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 10:50

Maelfu ya wafanyakazi wa afya watumwa Shanghai kupambana na Covid


Waganyakazi wa afya wakusanyika mbele ya bambo lenye maandishi yanayosema "tuungane katika vita dhidi ya janga ili tulishinde nguvu" Picha: AP

Serikali ya China imetuma maelfu ya wafanyakazi wa afya na wa kijeshi katika mji wa Shanghai, katika jaribio la kudhibithi wimbi jipya la maambukizi ya virusi vya Corona, huku mji huo ukiwa umepiga marufuku shughuli za kawaida kwa wiki ya pili sasa.

Kulingana na gazeti la jeshi la China, zaidi ya wafanyakazi wa afya 2,000 wanaofanya kazi katika jeshi hilo, wametumwa mjini humo kupambana na Corona.

Zaidi ya wafanyakazi wa afya 10,000 kutoka mikoa mingine wanatarajiwa kuwasili Shanghai hii leo.

Wanatoa huduma ya kupima, kutibu na kushughulikia matatizo mengine yanayohusiana na virusi vya Corona katika mji huo wenye jumla ya watu milioni 26.

Idadi hiyo ya maafisa wa afya ndio kubwa zaidi kuwahi kutumwa katika sehemu moja nchini China.

Mji wa Shanghai umeripoti visa 425 vya maambukizi ya virusi vya Corona vilivyothibitishwa katika mda wa saa 24, na zaidi ya 8,500 walioambukizwa virusi hivyo lakini hawaonyeshi dalili.

China inatekeleza kanuni kali sana za kupambana na maambukizi ya virusi vya orona, ikiwemo upimaji, kutafuta waliokaribiana na wagonjwa, walioambukizwa kukaa nyumbani na kujitenga, pamoja na kudhibithi maambukizi hayo katika mipaka yake.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG