Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 03, 2024 Local time: 13:42

Maelfu ya raia wa Lebanon wakimbilia Syria kutokana na vita kati ya Israel na Hezbollah


Watu waonekana kwenye lori dogo wakikimbia mapigano kati ya Israel na Hezbollah, Septemba 24, 2024. Picha ya AFP
Watu waonekana kwenye lori dogo wakikimbia mapigano kati ya Israel na Hezbollah, Septemba 24, 2024. Picha ya AFP

Familia zinazokimbia mzozo unaopamba moto nchini Lebanon ziliingia kwa wingi Jumatano nchini Syria, zikisubiri kwa saa kadhaa katika msongamano wa magari kupata usalama mdogo katika nchi hiyo nyingine inayokumbwa na vita.

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wanakadiria kwamba maelfu ya familia za Waleban na Wasyria tayari wamekimbia. Idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka wakati Israel imeshambulia eneo la kusini mwa Lebanon katika mashambulizi ya mabomu kwa kutumia ndege, ambayo maafisa wa eneo hilo wamesema yameua zaidi ya watu 600 wiki hii, robo yao wakiwa wanawake na watoto.

Israel inasema inalenga wapiganaji wa Hezbollah na zana zao.

Forum

XS
SM
MD
LG