Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 02, 2022 Local time: 12:27

Maelfu ya raia Czech wakusanyika kuonyesha mshikamano wao na Ukraine


Maelfu ya raia wa Czech watu walikusanyika kwenye maandamano ya kupinga vita huko Prague, Jamhuri ya Czech, Jumapili, Oktoba 30, 2022. (AP)

Maelfu ya raia Czeck wamekusanyika katika mji mkuu ili kuonyesha mshikamano wao na Ukraine na kuunga mkono maadili ya kidemokrasia.

Maandamano ya Jumapili yalifanyika kufuatia maandamano matatu ya hivi karibuni dhidi ya serikali ambapo waandamanaji wengine walidai kujiuzulu kwa serikali ya muungano inayounga mkono na Magharibi ya Waziri Mkuu wa kihafidhina Petr Fiala kwa uungaji mkono wake kwa Ukraine.

Maandamano hayo ya awali pia yalipinga kupanda kwa bei ya nishati na kupinga uanachama wa nchi hiyo katika Umoja wa Ulaya na NATO. Siku ya Jumapili, waliojitokeza mjini Prague walipeperusha bendera za Czech, Ukraine na Umoja wa Ulaya na kuonyesha mabango yanayosomeka "Jamhuri ya Czech dhidi ya hofu" na "Tutasimamia hilo”.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG