Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 15:15

Maelfu waandamana Uhispania

Nchini Uhispania maelfu ya watu walifurika katika mitaa ya Madrid  Jumapili  kwa maandamano mkubwa sana dhidi ya serekali ya kikanda ya mji mkuu kuhusu huduma za afya.

Nchini Uhispania maelfu ya watu walifurika katika mitaa ya Madrid Jumapili kwa maandamano mkubwa sana dhidi ya serekali ya kikanda ya mji mkuu kuhusu huduma za afya.

Zaidi ya watu 250,000 waliandamana katikati ya mji, kwa mujibu wa serekali kuu ya Uhispania.

Waandaaji wamedai kuwa umati mkubwa wa watu uliojitokeza ulikuwa mkubwa zaidi ambao ulikuwa na maelfu ya watu.

Waandamanaji wengi walikuwa na mabango yakiwa na ujumbe kwa Uhispania kama, wanapenda haki kuwa afya ni haki ya binadamu.

Chama cha wafanyakazi wa sekta ya afya kiliongoza maandamano ambayo yaliungwa mkono na vyama vya mrengo wa kushoto, umoja wa wafanyakazi, na wananchi wa kawaida kwa kile wanacho kiona kuwa uharibifu katika mfumo wa huduma za afya unaofanywa na serekali ya kikonsevative ya eneo la Madrid.

XS
SM
MD
LG