Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 18, 2025 Local time: 17:48

Maelfu waandamana nchini Uturuki kuomba nyongeza ya mshahara


Bendera ya Uturuki
Bendera ya Uturuki

Maelfu ya watu waliandamana Jumamosi katika mji mkuu wa Uturuki Ankara kuomba nyongeza ya kima cha chini cha mshahara, huku wakiimba nyimbo za kuitaka serikali kujiuzulu wakipeperusha bendera za upinzani na taifa.

Serikali ilitangaza wiki hii kwamba kima cha chini cha mshahara katika mwaka 2025 kitakuwa sawa na lira 22,104 za Uturuki, ikiwa ongezeko la asilimia 30 ikilinganishwa na mwaka 2024.

Serikali ilisema iliweka kiwango hicho ili kudhibiti matumizi ya fedha na kuendelea kukabiliana na mfumuko wa bei.

Wafanyakazi wa Uturuki ambao wamekabiliwa na mzozo wa gharama ya maisha na mfumuko wa bei unaotarajiwa kuongezeka kwa asilimia 45 mwaka huu, walikuwa wameomba nyongeza ya asilimia 70.

Chama kikuu cha upinzani nchini Uturuki, CHP, kimesema maandamano hayo ya kuomba nyongeza ya kima cha chini cha mshahara yameonyesha kwamba Rais Tayyip Erdogan “ hajui ukweli wa hali halisi ya wananchi wa Uturuki.”

Forum

XS
SM
MD
LG