Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 01, 2022 Local time: 20:01

Maelfu waandamana Mexico


Watu wakiwa mitaani kwa maandamano ya kupinga mabadiliko ya tume ya uchaguzi ya Mexico, Jumapili, Novemba 13, 2022.

Maelfu ya watu waliingia katika mtaa muhimu wa jiji kuu la Mexico, kuandamana kupinga mapendekezo ya rais Andres Manuel Lopez Obrador ya mabadiliko ya tume ya uchaguzi.

Maandamano hayo ni makubwa zaidi katika kupinga moja ya juhudi za rais katika kipindi cha miaka minne alicho kuwepo madarakani.

Kujitokeza huko kwa wingi kwa watu kunakuwa tofauti kabisa na ukosowaji wa rais kwamba upinzani ni mdogo na unafanywa na kundi dogo la wapinzani.

Vyama vya upinzani na makundi ya kiraia yalitoa mwito wa raia wa Mexico kuandamana katika mji mkuu, na miji mingine.

Hatua hiyo ni kupinga mapendekezo ya mabadiliko ya masuala ya uchaguzi ambayo yatabadilisha tume ya uchaguzi moja ya taasisi zenye heshima na kuaminika sana.

Rais Obrador anaona taasisi hiyo kushikiliwa na watu wenye ushawishi, lakini wakosoaji wanasema mabadiliko hayo yataondoa nguvu yake ya kuwa huru na kuifanya kuwa ya kisiasa zaidi.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG