Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 15, 2024 Local time: 04:51

Maelfu waandamana Mali kupinga vikwazo vya ECOWAS dhidi ya serikali ya mpito


Wafuasi wakiwa na bango la rais wa mpito wa Mali, Kanali Assimi Goita, wakati wakishiriki maandamano ya kupinga viwazo dhidi ya Mali.Jan. 14, 2022. REUTERS/Paul Lorgerie
Bamako, Mali, Jan. 14, 2022.
Wafuasi wakiwa na bango la rais wa mpito wa Mali, Kanali Assimi Goita, wakati wakishiriki maandamano ya kupinga viwazo dhidi ya Mali.Jan. 14, 2022. REUTERS/Paul Lorgerie Bamako, Mali, Jan. 14, 2022.

Maelfu ya watu waliandamana katika mji mkuu wa Mali Bamako siku ya Ijumaa dhidi ya vikwazo vilivyowekwa na nchi jirani kwa  serikali ya mpito ya kijeshi kwa kujaribu kuongeza muda wake wa kutawala.

Maelfu ya watu waliandamana katika mji mkuu wa Mali Bamako siku ya Ijumaa dhidi ya vikwazo vilivyowekwa na nchi jirani kwa serikali ya mpito ya kijeshi kwa kujaribu kuongeza muda wake wa kutawala.

Watu walimiminika kwenye Uwanja wa Uhuru, wakiwa na mabango yanayosema kuanguka kwa ECOWAS na kuanguka kwa Ufaransa kupinga vikwazo vilivyowekwa na Jumuiya ya Kiuchumi ya mataifa ya Afrika Magharibi na kuungwa mkono na utawala za zamani wa kikoloni Ufaransa.

Utawala wa kijeshi ulichukua mamlaka katika mapinduzi ya mwaka 2020 na awali ulikubali kufanya uchaguzi mwezi Februari mwaka huu. Lakini umerudi nyuma na hivi karibuni ulipendekeza tarehe mpya ya Desemba mwaka 2025.

Hatua hiyo imelaaniwa kimataifa, lakini raia wengi wa Mali wanaendelea kumuunga mkono Rais wa mpito Assimi Goita, kanali wa jeshi ambaye kitendo chake cha kumpindua Ibrahim Boubacar Keita kilikuwa maarufu sana nchini humo.

Niko hapa kusema kwamba Mali ni ya kwanza kwa Wamali, sio ECOWAS au Ufaransa ambao watafanya maamuzi badala yetu, alisema Adama Cisse, mwalimu mwenye umri wa miaka 40 katika umati huo.

XS
SM
MD
LG