Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 03:32

Maelezo zaidi juu ya mashtaka yanayowakabili Warusi 13 Marekani


Naibu Mwanasheria Mkuu Rod Rosenstein akitangaza mashtaka yaliofunguliwa na Baraza la Mahakama dhidi ya wananchi wa Russia 13 na makampuni kadhaa ya Urusi Februari 16, 2018, Jijini Washington.
Naibu Mwanasheria Mkuu Rod Rosenstein akitangaza mashtaka yaliofunguliwa na Baraza la Mahakama dhidi ya wananchi wa Russia 13 na makampuni kadhaa ya Urusi Februari 16, 2018, Jijini Washington.

Baraza la Mahakama ya Serikali Kuu nchini Marekani linalochunguza kuhusika kwa Russia kuingilia uchaguzi wa 2016 limewafungulia mashtaka raia 13 wa nchi hiyo wakiwemo wafanyakazi 12 wa St Petersburg, kampuni yenye makao yake huko Russia.

Kampuni hii inafanya shughuli zake za mitandaoni kushawishi operesheni mbalimbali kwa niaba ya Moscow. Chini hapa ni maelezo zaidi ya mashtaka hayo.

Kosa la Kwanza: Njama za udanganyifu wa mitandaoni dhidi ya Marekani

Makampuni husika:
Internet Research Agency LLC, ambayo inajulikana pia kama Mediasintez LLC, Glavset LLC, Mixinfo LLC, Azimut LLC, Novinfo LLC

Concord Management and Consulting LLC

Concord Catering

Watu waliohusika:

Yevgeniy Viktorovich Prigozhin – Anayesimamia makampuni hayo. Yeye na makampuni haya “wametumia kiwango kikubwa cha fedha kupeleka mbele operesheni mbalimbali za taasisi hii na kuwalipa washtakiwa waliobakia pamoja na wafanyakazi wengine ambao hawakufunguliwa mashtaka, mishahara, marupurupu kwa kazi zao katika taasisi hiyo.

Watu wafuatao wamefunguliwa mashtaka kwa “kujifanya wao ni Wamarekani na kutengeneza utambulisho wa bandia,” wakimiliki kurasa za mitandao ya kijamii na makundi mbali mbali yaliyokusudiwa kuwavutia wafuatiliaji wa mitandao kutoka Marekani.

Makundi haya ya Russia na kurasa zao katika mitandao ya kijamii, ambazo zilikuwa zikionyesha mgawanyiko wa siasa za Marekani na masuala ya kijamii, zilidanganya kuwa zinamilikiwa na wanaharakati wa Kimarekani wakati ukweli ni kuwa zilikuwa zinamilikiwa na washtakiwa hawa (kutoka Russia).

Washtakiwa hawa pia walighushi majina halisi ya watu wa Marekani na kuposti katika taasisi mbalimbali chuki hizo- katika akaunti za mitando ya kijamii zenye udhibiti.

Baada ya muda, akaunti hizi za mitandao ya kijamii zikawa ni njia ya washtakiwa hao kufikia idadi kubwa ya wananchi wa Marekani kwa minajili ya kuingilia kati mfumo wa kisiasa wa Marekani, ikiwemo uchaguzi wa urais wa 2016.

Mikhail Ivanovich Bystrov

Mikhail Leonidovich Burchik, pia anajulikana kama Mikhail Abramov

Aleksandra Yuryevna Krylova

Anna Vladislavovna Bogacheva

Sergey Pavlovich Polozov

Maria Anatolyevna Bovda, pia anajulikana kama Maria Anatolyevna Belyaeva

Robert Sergeyevich Bovda

Dzheykhun Nasimi Ogly (cq) Aslanov, pia anajulikana kama Jayhoon Aslanov, pia anajulikana kama Jay Aslanov

Vadim Vladimirovich Podkopaev

Gleb (cq) Igorevich Vasilchenko

Irina Viktorovna Kaverzina

Vladimir Venkov

Shtaka la Pili: Njama ya udanganyifu wa fedha kupitia mitandaoni

Internet Research Agency LLC

Dzheykhun Nasimi Ogly Aslanov

Gleb Igorevich Vasilchenko

Counts Three through Eight: Aggravated Identity Theft

Shtaka la Tatu mpaka la Nane: Kughushi utambulisho

Internet Research Agency LLC

Dzheykhun Nasimi Ogly Aslanov

Gleb Igorevich Vasilchenko

Irina Viktorovna Kaverzina

Vladimir Venkov

XS
SM
MD
LG