Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 23:03

Madeleine Albright afariki dunia


Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani Madeleine Albright akitoa hotuba huko Shanghai China wakati wa uhai wake.
Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani Madeleine Albright akitoa hotuba huko Shanghai China wakati wa uhai wake.

Waziri wa mambo ya nje wa kwanza mwanamke wa Marekani, Madeleine Albright amefariki kutokana na saratani, familia yake ilisema Jumatano. Alikuwa na umri wa miaka 84.

Waziri wa mambo ya nje wa kwanza mwanamke wa Marekani, Madeleine Albright amefariki kutokana na saratani, familia yake ilisema Jumatano. Alikuwa na umri wa miaka 84.

Rais Bill Clinton alimchagua Albright kama mwanadiplomasia mkuu wa Marekani mwaka 1996, na alihudumu katika nafasi hiyo kwa miaka minne ya mwisho ya mwisho ya utawala wa Clinton. Kabla ya hapo alikuwa balozi wa Clinton katika Umoja wa Mataifa.

Wakati huo, alikuwa mwanamke wa cheo cha juu zaidi katika historia ya serikali ya Marekani. Hakuwa katika nafasi ya kuwania kiti cha urais kwa sababu alikuwa mzaliwa wa Prague.

Alikuwa amezungukwa na familia na marafiki, familia yake ilitangaza kwenye Twitter. "Tumepoteza mama mwenye upendo, bibi, dada, shangazi na rafiki." Ilisema sababu ni saratani.

Mwaka 2012, Rais Barack Obama alimtunukia Albright nishani ya Uhuru, heshima ya juu zaidi ya kiraia, akisema maisha yake yalikuwa msukumo kwa Wamarekani wote.

Hata hivyo, Albright, ambaye alitoroka Wanazi akiwa mtoto katika nchi yake ya asili ya Czechoslovakia wakati wa Vita vya Pili vya Dunia aliibuka kuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani wa kwanza mwanamke na, katika miaka yake ya baadaye, mwanaharakati wa masuala ya wanawake wa utamaduni wa Marekani.

Albright alikuwa mwanadiplomasia mwenye kuchukua maamuzi magumu katika utawala ambao ulisita kujihusisha katika mizozo mikubwa miwili ya sera za nje ya miaka ya 1990 katika mauaji ya kimbari nchini Rwanda na Bosnia-Herzegovina.

Albright alikuwa balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa kuanzia 1993 hadi 1997 na waziri wa mambo ya nje wakati wa Rais Bill Clinton kuanzia 1997 hadi 2001.

XS
SM
MD
LG