Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 30, 2023 Local time: 01:55

Madaraka ya rais wa Afrika kusini yaimarika baada ya kuchaguliwa kuongoza ANC


Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa

Ramaphosa alichaguliwa tena, na kumtengenezea njia ya kugombea muhula wa pili wa urais mwaka 2024, Jumatatu katika kura ya wanachama wa African National Congress -ANC ambayo pia ilichagua wajumbe wapya wa mkutano wa halmashauri kuu ya taifa ya chama hicho -NEC.

Upigaji kura huo uliwaweka kando baadhi ya mawaziri na wengine katika kambi ya kumpinga Ramaphosa ambayo ina uhusiano na Jacob Zuma ambayo, pamoja na rais huyo wa zamani aliyejiingiza katika kupambana na madai ya ufisadi ambayo anayakanusha, aliungana na waziri wa zamani wa afya Zweli Mkhize.

Afrika kusini imekumbwa na changamoto za kisiasa mwishoni mwa mwaka huu ambazo wachambuzi wa mambo wanasema zilipelekea kuzorota kwa harakati nyingi katika serikali ya nchi hiyo.

Hata hivyo mara baada ya kuchaguliwa tena kuwa kiongozi wa ANC Ramaphosa aliahidi kuendelea kupambana kuinua uchumi wa nchi hiyo na huduma msingi kama vile afya .

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG