Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 02:36

Madaktari wasio na mipaka waonya juu ya upatikanaji wa huduma za ARV Congo.


Wanawake wa Congo.(AP Photo/John Bompengo)
Wanawake wa Congo.(AP Photo/John Bompengo)

Madaktari wasio na mipaka waonya juu ya upatikanaji wa huduma za ARV Congo.

Kundi moja la madaktari limeonya kwamba mpaka waathirika 15,000 wa Ukimwi katika jamhuri ya kudemokrasia ya Congo wanaweza kupoteza maisha katika miaka mitatu ijayo kwasababu ya ugumu wa kupata dawa za kuokoa maisha.

Onyo hilo limetolewa na madaktari wasio na mipaka ambao wanasema upatikanaji wa huduma za afya kwa wagonjwa wa HIV na AIDS huko Congo ni mbaya sana.

Imesema asilimia 85 ya watu wanaokadiriwa 350,000 ambao wangeweza kupata faida kutoka kwenye dawa za anti retroviral (ARV) hawapati dawa hizo.

XS
SM
MD
LG