Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 15:30

Madaktari waanza mgomo Kenya


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta

Madaktari wanaofanya kazi katika hospitali za serikali nchini Kenya, wameanza mgomo wa kote nchini hii leo, wakilalamikia kutopewa bima ya afya, na ukosefu wa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona wanapowashughulikia wagonjwa walioambukizwa virusi hivyo.

Mgomo huo umeanza leo baada ya muungano wa madaktari, wanafamasia na madaktari wa meno kusema kwamba serikali imekosa kushughulika mahitaji yao kwa mda wa miezi nane iliyopita.

Muungano huo umesema kwamba serikali ya Kenya imepuuza maslahi ya wafanyakazi wa afya nchini humo.

Kulingana na muungano huo, madkatari 14 wamekufa kutokana na virusi vya Corona nchini Kenya, tangu kisa cha kwanza kiliporipotiwa mwezi Machi mwaka huu.

Mgomo huo ulikuwa umepangiwa kuanza Desemba 7 lakini ukaahirishwa kwa mda wa wiki mbili ili kuruhusu mazungumzo kati ya viongozi wa madaktari na serikali, kufanyika.

Maambukizi ya virusi vya Corona yamekuwa yakiongezeka katika sehemu za mashambani ambapo mfumo wa afya sio mzuri.

Kenya imeripoti maambukizi ya Corona kati ya watu 349 na vifo 6 hii leo.

Jumla ya watu 94,500 wameambukizwa Corona nchini Kenya.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG