Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 03, 2022 Local time: 21:58

Madai ya Ufisadi : Gavana wa Nairobi kufikishwa mahakamani Jumatatu


Gavana Mike Sonko

Gavana wa Nairobi Mike Sonko alifanya ukaidi kujaribu kukimbia abakie huru mapema siku ya Ijumaa.

Lakini kutokana na dosari kadhaa alizozifanya na wasaidizi wake akijaribu kukwepa kukamatwa kulifanya kukimbia kwake kuishie ukingoni kwani alikamatwa huko Voi, kilomita 300 kutoka Nairobi, wakati akiwa ndani ya gari anaelekea Mombasa..

Uamuzi wa kumkamata ulifikiwa siku mbili zilizopita lakini ilichukua masaa 11 yaliyokuwa na vioja vya hali ya juu hadi polisi wa kikosi maalum kumfikia na kumdhibiti.

Anashutumiwa pamoja na mambo mengine, kutumia madaraka vibaya, na anakabiliwa na mashtaka ya ufisadi ya zabuni zinazotolewa mjini Nairobi.

Mkurugenzi wa Mashtaka ya Jinai Noordin Haji amewaambia waandishi wa habari jijini kuwa Sonko na washirika wake walikuwa wanaendesha mfumo wa ufisadi uliopelekea ubadhirifu wa kiasi kisichopungua shilingi milioni 357.

Kufuatia kukamatwa kwake, anatarajiwa kufikishwa mahakamani Jumatatu.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG