Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 30, 2024 Local time: 21:43

Madagascar imewakamata washukiwa zaidi wa njama za kumuua Rais Andry Rajoelina


Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina
Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina

Taatifa inaeleza washukiwa 21 wakiwemo wanajeshi 12 walikamatwa kuhusiana na njama za kutaka kumuua Rais Rajoelina.

Madagascar imewakamata washukiwa wengine 21 wakiwemo wanajeshi 12 kuhusiana na njama ya kumuua Rais Andry Rajoelina na kuiangusha serikali mwendesha mashtaka mwandamizi alisema.

Watu sita mmoja wao ni raia wa Ufaransa walikamatwa mwezi uliopita kwa tuhuma za kuhusika na njama hiyo kufuatia kile maafisa walichoelezea kuwa uchunguzi wa miezi kadhaa katika kisiwa hicho kilichopo bahari ya Hindi.

Wanajeshi waliokamatwa ni pamoja na majenerali watano kutoka jeshini, na manahodha wawili, na maafisa watano ambao hawajapewa kazi, alisema jana Jumapili, mwendesha mashtaka wa mahakama ya rufaa ya Antananarivo, Berthine Razafiarivony. Hata hivyo hakutaja majina yao.

XS
SM
MD
LG