Ofisi ya Macron imesema ziara yake inalenga kuweka msingi wa kujenga upya na kuendeleza uhusiano wakati mwingine mgumu na taifa hilo la Afrika kaskazini baada ya miezi michache ya mvutano.
“Hatukuchagua yaliyopita, tuliyarithi,” amesema katika mkutano na waandishi wa habari Alhamisi pamoja na Rais wa Algeria Abdelmajid Tebboune.
“Lazima tuiangazie hali hii na kuitambua, lakini tuna wajibu wa kujenga mustakabali wetu kwa ajili yetu na vijana wetu,” amesema Macron, akiwa rais wa kwanza wa Ufaransa aliyezaliwa tangu uhuru wa Algeria mwaka wa 1962.
Tebboune amepongeza “mwelekeo huo mzuri” katika uhusiano wa nchi hizo mbili, akisema kuna “ matarajio mazuri ya kuboresha ushirikiano maalum ambao unatuunganisha”.
Rais wa Ufaransa ametangaza Alhamisi jioni kwamba nchi hizo mbili zitaunda tume ya pamoja ya wanahistoria wa Ufaransa na Algeria kuchunguza nyaraka kuhusu miaka 130 ya utawala wa kikoloni wa Ufaransa nchini Algeria, ikiwemo vita vibaya vya miaka minane vya uhuru.