Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 19, 2025 Local time: 05:43

Macron aomba wanahistoria kuchunguza maovu yaliyotendwa enzi ya ukoloni nchini Cameroon


Rais wa Cameroon Paul Biya akipeana mkono na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron kwenye ikulu mjini Yaounde, Julai 26, 2022. Picha ya Reuters
Rais wa Cameroon Paul Biya akipeana mkono na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron kwenye ikulu mjini Yaounde, Julai 26, 2022. Picha ya Reuters

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron Jumanne amesema nyaraka za kumbukumbu kuhusu utawala wa kikoloni wa Ufaransa nchini Cameroon zitawekwa wazi “kikamilifu” na amewaomba wanahistoria kutoa mwanga kuhusu “nyakati za uchungu” za kipindi hicho.

Macron, akizungumza katika mji mkuu wa Cameroon Yaounde, amesema anataka wanahistoria kutoka nchi hizo mbili kushirikiana kwa kuchunguza yaliyotokea miaka ya nyuma na kubaini “wahusika”.

Viongozi wa kikoloni wa Ufaransa waliwakandamiza kikatili watetezi wa uhuru wa Cameroon waliokuwa na silaha kabla ya uhuru wa nchi hiyo mwaka wa 1960.

Maelfu ya wafuasi wa chama cha Union of the Peoples of Cameroon (UPC), akiwemo kiongozi wa uhuru Ruben Um Nyobe, waliuawa na jeshi la Ufaransa.

XS
SM
MD
LG