Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 00:42

Watu 22 wameuwawa kwa mabomu Nigeria

Watu wakikagua msikiti kufuatia mlipuko uliotokea Maiduguri, Nigeria, Oct. 23, 2015.
Watu wakikagua msikiti kufuatia mlipuko uliotokea Maiduguri, Nigeria, Oct. 23, 2015.

Mmoja aliripotiwa kuingia ndani ya msikiti mapema leo katika mtaa wa Umarari na kutegua bomu lake wakati mwingine akisubiri nje na alitegua mlipuko wake wakati watu wanakimbia nje ya jengo hilo.

Wajitomhanga wamelipua mabomu wawili na kuuwa watu wasiopungua 22 na kuwajeruhi 17 wengine kwenye msikiti mmoja nje ya Maiduguri huko Nigeria. Walioshuhudia wanasema walipuaji walikuwa wanawake waliova ngu za kiume.

Mmoja aliripotiwa kuingia ndani ya msikiti mapema leo katika mtaa wa Umarari na kutegua bomu lake wakati mwingine akisubiri nje na alitegua mlipuko wake wakati watu wanakimbia nje ya jengo hilo.

Kundi la wanamgambo wa Boko Haram lilianzishwa mjini Maidiguri na umekua kiinchio cha serikali katika kupambana kulitokomeza kabisa kundi hilo la kiislam ambalo limefanya mashambulizi mengi huko kaskazini mwa Nigeria na nchi jirani kuzunguka ziwa Chad: Niger, Chad na Cameroon. Hakuna mtu au kundi lolote linalodai kuwajibika kwenye mlipuko wa leo.

XS
SM
MD
LG