Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 09, 2022 Local time: 16:32

Mabasi mawili yachomwa kwenye mgomo Afrika Kusini.


Gari lililochomeka Afrika kusini kwenye picha ya maktaba.

Mabasi mawili  yamechomwa moto Jumatatu kwenye mji wa  Cape Town, Afrika kusini, kufuatia mgomo wa siku mbili uliyoitishwa na makampuni ya wamiliki wa magari ya kubeba umma.

Washiriki wanalalamikia kusitishwa kwa program ya ruzuku iliyolenga kuwasadia madereva wanaoendesha kwa makini pamoja na wale wanaojiepusha na utovu wa nidhamu.

Program hiyo imesitishwa na serikali ya jimbo la Western Cape kutokana na uhaba wa fedha, baada ya kuwepo kwa zaidi ya mwaka mmoja. Foleni ndefu zimeshuhudiwa kwenye vituo vya mabasi kuanzia saa za asubuhi, wakati wa watu kwenda kazini, pamoja na wanafunzi kwenda shule.

Mtu mmoja miongoni mwa waandamanaji anesemekana kushambulia moja ya mabasi yaliyochomwa, kwa kutoboa matairi yake, ili kulizuia kubeba abiria. Watu waliyokuwa ndani walilazimika kuruka kupitia kwenye madirisha , huku mwanamke mmoja akiachwa na majeraha.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG